Yaliyojiri leo kwenye usajili Barani Ulaya.


Mshambuliaji wa Dortmund Emerick-Pierre Aubameyang atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Serie A endapo atajiunga na AC Milan.

Kyle Walker atakuwa ndiye beki ghali zaidi kwa sasa duniani endapo atasajliwa Man City kwa dau la pauni 54 milioni.

Chelsea imeanza kupoteza matumaini ya kumsajili Leonardo Bonucci ambaye atajiunga na AC Milan ya Italy.

Manchester United inajipanga kuwatoza Real Madrid kiasi cha pauni 50 milioni kama ada ya uhamisho wa golikipa David De Gea.

Liverpool imetolewa na RB Leipzing licha ya kufikia dau pauni 57 milioni kumsajili kiungo Naby Keita.

Chelsea huenda ikawa imekalisha dili la kumsajili kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko ambaye tayari alipost usajili hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Everton inajipanga kufanya usajili mwingine mkubwa ambapo itatoa kiasi cha pauni 40 milioni kumsajili Gylfi Sirgurdsson wa Swansea.

Comments