Yaliyojiri leo kwenye usajili barani Ulaya.


Golikipa wa Manchester City Joe Hart anajiandaa kukamilisha zoezi la vipimo jumatatu ya leo ili kuijunga na West Ham United kwa mkopo.

Hart mwenye miaka 30 alijiunga na Torino kwa mkopo msimu ulioisha baada ya baada ya kusajiliwa golikipa Claudio Bravo kutoka Barcelona.

Hata hivyo golikipa huyo amefikia maamuzi hayo baada ya Pep Gurdiola kumsajili golikipa wa Brazil Ederson aliyetokea Benifica ya Ureno.
Na kwa upande mwingine msahabuliaji wa 


Manchester City Nolito amajiunga na Sevilla na kwa ada ya uhamisho wa pauni 7.9 milioni.
Nolito alisajiliwa na Gurdiola akitokea Celta Vigo kwa dau la pauni 13 milioni hata hivyo ameshindwa kufua dafu mbele ya Leroy Sane ambaye amekuwa chaguo namba moja la Gurdiola dhidi ya Nolito.

                              Liverpool

Beki wa Southampton Virgil Van Djik ana imani Liverpool itakubali dau la pauni 60 milioni ili nyota huyo atue Anfield.

Comments