Yaliyojiri leo kwenye usajili barani Ulaya


PSG ipo mbioni kuweka mezani kiasi cha pauni 196 milioni ili kukamilisha usajili wa Neymar kutoka Barcelona. Kwa upande wa Barcelona wameonekana kushawishika na dau hilo.

Alexis Sanchez ameitaka PSG kumlipa kiasi cha pauni 500,000 kwa wiki endapo atajiunga na timu hiyo.

Barcelona imeijaribu tena Liverpool kwa kiungo wake Phelipe Coutinho baada ya kuweka mezani ofa ya pauni 80 milioni.

Riyad Mahrez amekataa ofa ya kujiunga na AS Roma na ameitaka timu hiyo imuuze Arsenal kwa dau la pauni 35 million ambalo pia limefikiwa na Roma.

West Brom inajianga kumsajili kiungo Moussa Sissoko ambaye amepwaya tangu alipojiunga na Tottenham.

Kocha wa Everton Ronald Koeman bado ataendelea na usajili hadi atakapofikia kiasi cha matumizi ya pauni 130 milioni.

Manchester United inajiandaa kupeleka ofa ya pauni 60 milioni kwa PSG ili kumsajili Verrati ambaye ameonesha nia ya kujiunga na Man utd.

Comments