Timu ya Borrusia Dortmund inataka kumsajili Mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud baada ya kuthibitisha kuwa ataondoka Emirates.
Kocha wa Manchester city Pep Guardiola amekataa ofa ya PSG kwa ajili ya kumnunua kiungo Yaya Toure.
Baada ya kumkosa Lukaku Chelsea imeanza kujipanga ili kumnasa Mshambuliaji wa Dortmund Pierre Emerick Aubameyang.
Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs Daniel Levy ameitaka Manchester city kutoa kiasi cha pauni 50 milioni ili kumsajili beki wa kulia Kyle Walker.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anajipanga kupeleka ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Angel Correa.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kukamalisha kiasi cha pauni 100 milioni katika usajili baada ya kupeleka ofa ya kumsajili kiungo Thomas Lemar kutoka Monaco.
Timu ya Lazio inataka kuanza mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya kumsajili kiungo wake Lucas Leiva ambaye pia anahusishwa na Besiktas.
Manchester United inatakiwa kutoa kiasi cha pauni 50 milioni kama inahitaji kumsajili kiungo na mlinzi wa Tottenham Eric Dier.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anataka kuongeza mshahara wa kiungo Ander Herrera kufikia kiasi cha pauni 175000 kwa wiki ili kuzikata maini Barcelona na Atletico Madrid ambazo zinamtolea macho kiungo huyo.

Comments
Post a Comment