Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC imeamua kuachana na golikipa wake namba moja Deogratius Munish 'Dida'.
Hayo yamesemwa na kocha wa makipa katika klabu ya Yanga Juma Pondamali ambaye alikuwa akifanya mahojiano na radio one.
Dida aligoma kuongeza mkataba kwenye klabu hiyo kutokana na madai ya kwenda majaribio kwenye nje ya Tanzania.
Golikipa huyo aliwataka Yanga kumpa mkataba mwingine endapo atashindwa kufuzu majaribio yake jambo ambalo limepingwa na uongozi wa Yanga.

Comments
Post a Comment