Aggrey, Sure Boy waongeza mkataba Azam.


Beki wa Azam FC na Kiungo Sure Boy wameongeza mkataba wa mwaka kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Makamu mwenyekiti wa Azam Abdulkarim Mohamed ndiye aliyesimamia zoezi zima la kumwaga wino kwa wachezaji hao.

Morris na Sure Boy walibakiza mwaka mmoja kila mmoja lakini mkataba mpya utawafanya kudumu kwenye timu hiyo hadi mwaka 2019.

Uongozi wa Azam kwa kushirikiana na benchi la ufundi wameamua kuwaongeza mkataba wachezaji hao kutokana na kiwango bora wanachokionesha.

Sure Boy na Morris ni moja kati ya wachezaji wakongwe ambao wamedumu na timu hiyo kwa zaidi ya misimu sita, 

Morris alijunga na timu hiyo mwaka 2009 akitokea Mafunzo ya Zanzibar, na Sure yupo na Azam kabla haijapanda daraja mwaka 2008.

Comments