Arsenal ipo kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kuamua hatma ya mshambuliaji wa timu hiyo Oxlade Chamberlain mpaka sasa.
Chamberlain amegoma kusaini mkataba mpya jambo ambalo linaipa wakati mgumu kama mchezaji anataka kuondoka kuondoka au huenda akabaki.
Chelsea ndiyo inayoongoza kwenye mbio za kumwania mchezaji huyo ambaye thamani yake inaweza kufikia hadi Pauni 50 milioni.
Chamberlain mwenye miaka 24 ataondoka akiwa mchezaji huru endapo hataweza kusaini mkataba mpya kutokana na kubakiza mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo.

Comments
Post a Comment