Mshambuliaji anayekuja kwa kasi katika medani ya soka Marco Asensio ndiye aliyeichomoa Real Madrid kwenye kipigo baada ya kufunga mabao muhimu dhidi ya Valencia.
Asensio alianza kutikisa nyavu za Valencia katika dakika ya 10 lakini Valencia walichomoa bao hilo katika ya 18 ya mchezo huo kupitia Carlos Soler.
Kipindi cha pili Real Madrid walionekana kutawala zaidi mpira na kasi yao iliongezeka lakini ujanja wa kiungo Geoffrey Kondogbia aliwazidi ujanja mabeki wa Madrid na kufunga bao la pili katika dakika ya 77.
Asensio 21, ambaye kwa sasa ameaminiwa sana na Zinedine Zidane aliweza kuinasua Madrid kwenye kipigo baada ya kuchomoa bao hilo katika dakika ya 83.
Marco Asensio ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo licha ya Real Madrid kukubali kuachia pointi 2 muhimu katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Comments
Post a Comment