Azam FC ipo njiani kuifata Ndanda Mtwara.


Timu ya Azam FC tayari imeondoka Dar es Salaam kuelekea Mtwara kuanza maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom itakayoanza jumamosi hii.

Azam itafungua dimba na Ndanda FC Siku ya jumamosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani.

Timu hiyo iliweka kambi ya siku 10 nchini Uganda kujiandaa na ligi kuu Vodacom ambapo iliweza michezo minne ya kirafiki dhidi ya Vipers, KCCA na The cranes ya wachezaji ya Ndani.

Azam ina kumbukumbu ya kupoteza mchezo katika uwanja huo msimu uliopita baada ya kufungwa na Ndanda bao 1-0.

Comments