Azam imevunja mwiko Mtwara, waichapa Ndanda 1-0.


Azam FC imeanza na ushindi hapo jana katika ufunguzi wa ligi kuu Vodacom baada ya kuichapa Ndanda FC bao 1-0 katika uwanja wa Nangwanda sijaona.

Azam ilipata bao la ushindi katika dakika ya 36 baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Yahya Mohamed kuunganisha kwa kichwa krosi safi iliyopigwa na Bruce Kangwa.

Kwa muda wa miaka 3 hatimaye Azam imeweza kupata ushindi katika uwanja huo ambao mara kadhaa wamekuwa wakipoteza mchezo au kuambulia sare.

Mbali na mchezo huo pia Singida United ilianza vibaya ligi kuu baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mwadui.

Comments