Azam FC imetangaza kumaliza na Kagera Sugar kuhusiana na sakata la usajili wa Mbaraka Yusuph baada ya kupokea barua ya makubaliano kutoka Kagera.
Usajili wa mshambuliaji huyo uliingia doa baada ya Kagera kuilalamikia Azam kumsainisha Mbaraka hali ya kuwa yupo bado ana mkataba na timu hiyo.
Azam kupitia msemaji wake Jaffar Idd imethibitisha kumalizana na Kagera hapo jana baada ya kufanya kikao ambacho kilifikia mwafaka wa suala hilo.
"Jana tulikuwa na kikao na Kagera Sugar, tayari tumefikia mwafaka wa suala hilo na Mbaraka ni mchezaji halali wa Azam." Alisema Msemaji huyo.

Comments
Post a Comment