Azam kuweka kambi nchini Uganda.


Timu ya Azam FC inajiandaa kuweka kambi ya siku 10 nchini Uganda kuanzia Agosti 6 mwaka huu.

Azam kupitia msemaji wake Jaffar Idd amethibitisha kuwa kikosi hicho kitapaa kuelekea Uganda kwa ajili kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi kuu Agosti 26 mwaka huu.

Mabingwa hao wa kombe la mapinduzi wanatakuwa na kibarua kizito cha kusaka pointi 3 dhidi ya Ndanda katika mchezo wa ufunguzi utakaopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Azam itacheza mechi nne za kirafiki nchini Uganda dhidi ya Sports Villa, KCCA, Vipers na URA.

Comments