Mabingwa wa kombe la Kagame Azam FC leo watashuka dimbani kwa mara nyingine katika mchezo wa kirafiki dhidi URA ya Uganda.
Huo ni mchezo wa pili kwa Azam ambayo imeweka kambi kwa muda wa siku 10 baada ya kutoka sare katika mchezo wa jana dhidi ya KCCA.
Pia Azam itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers Agosti 14 mwaka huu kabla ya kurejea nyumbani kwa maandalizi ya mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda sijaona.

Comments
Post a Comment