Azam FC imeendelea kuimarisha kikosi chake katika kambi waliyoweka nchini Uganda baada ya hapo jana kuichapa URA ya Uganda bao 2-0 katika uwanja wa Philip Omondi.
Mabao ya Azam yalifungwa na mshambuliaji yahya Mohamed katika kipindi cha kwanza kwenye dakika ya 19 na kipindi cha pili dakika ya 47.
Tayari Azam imecheza michezo miwili mpaka sasa na pia itamaliza mchezo wa mwisho dhidi ya Vipers kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho.
Azam itarejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya siku 10 nchini Uganda.

Comments
Post a Comment