Baada ya kufuzu kwenye makundi UCL, Liverpool yakimbilia kumsajili Sanchez


Baada ya kufuzu kwenye hatua ya makundi ya ligi ya hatimaye zimeibuka tetesi kuwa Liverpool inamnyemlea kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez.

Liverpool imewang'oa Hoffenheim baada ya kuifunga jumla ya mabao 6-3 katika mchezo wa nyumbani na ugenini.

Mapema leo meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametangaza kuwa timu inajipanga kuingia sokoni ili kuimarisha kikosi kwa ajili ya mapambano ya ligi hiyo ngumu.

Hadi sasa hatma ya kiungo Phelipe Coutinho haileweki kwenye kikosi hicho kutokana na kuomba timu hiyo imkubalie kujiunga na Barcelona.

Pia Liverpool inalazimika kuingia sokoni kutokana na kumkosa Adam Lallana ambaye atakaa nje kwa muda wa miezi miwili kutokana na majeraha.

Comments