Bailly: Ramos ndiye shujaa wangu uwanjani.


Beki wa Manchester United Eric Bailly amesema kuwa linapokuja suala la ulinzi uwanjani amejifunza mambo mengi kupitia mkongwe wa Real Madrid Sergio Ramos.

Bailly mwenye miaka 23 amesema kuwa mara nyingi amekuwa akimtamzama Sergio Ramos na kujifunza vitu vingi kutoka kwake.


                         Sergio Ramos

Beki huyo ambaye kwa sasa ni kipenzi cha mashabiki wa Manchester United pale Old Trafford amesema kuwa na ndoto za kuvaa viatu vilivyoachwa na Rio Ferdinand pamoja na Nemanja Vidic.

Bailly amedai kuwa tangu alipokuwa mdogo alipenda kucheza nafasi nyingi uwanjani.

"Siku zote nilipendelea kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani tangu nilipokuwa mdogo." Anasema Bailly

"Na siku zote Ramos ndiye shujaa wangu, nina mtazama mara nyingi." Alisema Bailly.

Comments