Barcelona imethibitisha kumalizana na mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele wa ada tya uhamisho wa pauni 97 milioni.
Kwa mujibu wa Sky sports tayari mazungumzo baina ya pande hizo mbili yalikwenda vizuri na sasa wamefikia makubaliano.
Dembele mwenye miaka 20 atapaa kuelekea Barcelona siku ya jumatatu ambapo atahitajika kukamilisha zoezi la vipimo na kusaini mkataba wa miaka 5.

Comments
Post a Comment