Real Madrid imezid kuonesha cheche zake chini ya kocha wa sasa Zinedine Zidane baada ya kutwaa taji la Super Copa dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
Mchezo huo ulihitimishwa jana baada ya Barcelona kupokea tena kipigo cha mabao 2-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Washambuliaji Marco Asensio na Karibu Benzema walitosha kuimaliza Barcelona hapo jana baada ya kufunga mabao ya ushindi.
Real Madrid ilishuka dimbani jana bila nyota wake Christiano Ronaldo ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Camp Nou.
Barcelona ilikamilisha kipigo cha mabao 5-1 hapo jana baada ya kufungwa bao 3-1 katika mchezo wa kwanza.



Comments
Post a Comment