Cannavaro: Bahati haikuwa kwetu.


Beki mkongwe wa klabu ya Yanga Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro amesema klabu ya Yanga haikuwa na bahati siku ya jana katika mchezo kwa ngao hisani dhidi ya Simba.

Simba ilipata fursa ya kunyakua ngao jamii baada ya kuibuka kidedea kwenye mikwaju ya Penati ambapo ilipata penati 6-5.

Akizungumza jana baada ya mechi hiyo Cannavaro alisema kuwa Yanga walicheza vizuri sana isipokuwa bahati haikuwa kwao.

"Timu imecheza vizuri sana, tena sana." Anasema Cannavaro ambaye alionekana kufurahishwa na kiwango ambacho Yanga ilikionesha hapo jana.

"Hakuna ubishi timu ilikuwa vizuri, hata wachezaji wapya wameonesha uwezo was hali ya juu, naisifu timu yangu kwa kucheza mpira mzuri." Aliongeza Cannavaro.

Katika mechi hiyo kiungo mpya wa klabu ya Yanga Papy Kabamba Tshimbimbi alionesha kiwango kizuri na kuteka hisia za wapenzi soka.

Comments