Mshambuliaji wa Arsenal Alex-Oxlade Chamberlain ametupa chini mpango wa kujiunga na Chelsea ambayo ipo mstari wa mbele kumwania nyota huyo.
Chamberlain mwenye miaka 24 anavutiwa na mpango wa kujiunga na Liverpool licha ya Arsenal na Chelsea kufanya makubaliano ya pauni 35 milioni kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Winga huyo mwenye kasi atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu na chaguo lake kwa ni kusubiri kumalizika kwa miezi 11 ya mkataba wake au kujiunga na Liverpool.
Chamberlain alifanya mazungumzo na Meneja Arsene Wenger baada ya mchezo wa jumapili dhidi ya Liverpool ili kujua hatma yake ndani ya timu hiyo.

Comments
Post a Comment