Chelsea imempata atakayerithi mikoba ya Antonio Conte.


Timu ya Chelsea ipo mbioni kuachana na meneja was sasa Antonio Conte na nafasi itachukuliwa na Thomas Tuchel.

Tayari zipo habari kuwa Chelsea imeanza mazungumzo na Tuchel kutokana na kuendelea kwa sinfofahamu na meneja wao wa sasa.

Thomas Tuchel ndiye aliyekuwa kocha wa Borrusia Dortmund msimu uliopita na alitangaza kuachana na timu hiyo mwezi Mei.

Inasemakana Antonio Conte ambaye aliipatia Chelsea ubingwa wa ligi kuu ameshindwa kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo.

Gazeti la Chelsea The Sun limeripoti kuwa kocha huyo amekuwa na mahitaji mengi hali inayopelekea viongozi kumchoka raia huyo wa Italy.

Pia inasemekana Conte hana maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji ikiwemo Diego Costa waliyegombana siku za hivi karibuni.

Comments