Mabingwa ligi kuu England Chelsea imekubali ada ya uhamisho ya mshambuliaji wa Arsenal Alex-Oxlade Chamberlain kwa mujibu wa Sky sports.
Chamberlain mwenye miaka 24 amegoma kusaini mkataba mpya katika klabu yake ya sasa akishinikiza kuondoka Arsenal.
Tayari makubaliano binafsi baina ya Chelsea na mchezaji huyo yamefikiwa, kwa mujibu wa Sky sports Chamberlain atapokea kiasi cha £180000 kwa wiki.
Chamberlain atamaliza mkataba wake Arsenal mwishoni mwa msimu huu sambamba na wachezaji wenzake Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Comments
Post a Comment