Chelsea yampiga faini Diego Costa.


Chelsea imeamua kumtoza faini mchezaji wake Diego Costa baada ya kushindwa kuhudhuria kipindi chote cha kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Mchezaji huyo atakosa kiasi cha pauni 300,000 ambao ni mshahara wake wa wiki mbili baada ya kuonesha kitendo hicho cha utovu wa nidhamu.

Costa alifanya mahojiano na mwandishi wa gazeti la Daily Mail na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea Chelsea kwa sasa.

Costa mwenye miaka 28 alisema kuwa hatajali endapo Chelsea haitamlipa mshahara mchezaji kutokana na mpango wake wa kubaki Brazil kwa mwaka mzima.

Pia mchezaji huyo ameituhumu tiny hiyo kumnyima nafasi ya kujiunga na Atletico Madrid kama alivyotaka.

Kwa upande mwingine Costa anashangazwa na uongozi wa Chelsea ambao hautaki kumwachia licha ya kumwambia hayupo kwenye mipango ya kocha Antonio Conte.

Baada ya kumalizika kwa ligi ya England Costa alipokea ujumbe kutoka kwa meneja Antonio Conte mchezaji huyo hayupo kwenye hesabu zake.

Comments