Chirwa, Kakolanya wataukosa mchezo wa watani wa jadi.


Kuelekea mchezo wa ngao ya jamii Agosti 23 mwaka huu Yanga itawakosa nyota wake watatu katika mchezo huo dhidi ya wapinzani wao.

Kwa mujibu wa Dauda blog imeripoti kuwa Yanga kupitia msemaji wake Dismass Ten amethibitisha kuwa Obrey Chirwa, Geoffrey Mwashiuya na Ben Kakolanya hawatakuwa sehemu ya mchezo.

Yanga imepiga kambi visiwani Visiwani Pemba ikijiandaa na mtange huo wa ngao ya hisani bila wachezaji hao watatu.

"Ben Kakolanya, Geoffrey Mwashiuya na Obrey Chirwa hawatakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na kuuguza majeraha.

"Kwa mujibu wa Dkt Bavu amethibitisha wachezaji hao wataukosa mechi Agosti 23 mwaka huu." Alisema Ten.

Pia msemaji huyo aliongeza kuwa Yanga watarejea jijini  Agosti 22 ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.

Comments