Washambuliaji tishio wa Yanga Obrey Chirwa na Amis Tambwe wamerejea mazoezini baada ya kupata nafuu ya majeraha yaliyokuwa yanawakabili.
Kwa mujibu wa msemaji Yanga Dismas Ten amethibitisha kurejea kwa wachezaji hao baada ya kupata nafuu.
"Hali zao zinaendelea vizuri na wataendelea kuzitumikia mechi zijazo." Alisema Ten
Obrey Chirwa na Amis Tambwe walikosa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba na pia ule wa ufunguzi wa ligi kuu Vodacom dhidi ya Lipuli ya Iringa.

Comments
Post a Comment