City yaweka dau jipya kumng'oa John Evans


Manchester city inajiandaa kupeleka ofa mpya ya £35 milioni kuishawishi West Brom iwauzie John Evans.

Chanzo kimoja kimeripoti kuwa tayari city walipeleka ofa ya kwanza ya £18 miliono ambayo ilikataliwa na West Brom.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Manchester City imejipanga kupeleka ofa ya pili kwa West Brom ambayo imeweka ngumu kumuachia mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United.

Inaelezwa kuwa meneja wa Manchester City Pep Gurdiola anavutiwa  na utulivu wa beki huyo ambaye hana papara anapokuwa na mpira mguuni.

Comments