DONE DEALS: Ibrahimovic amesaini mwaka mmoja Man Utd.


Mshambuliaji Zlatan Ibrahomivic bado ataendelea kuitumikia Manchester United kwa msimu mwingine baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Raia huyo wa Sweden anaendelea vizuri baada ya kuuguza majera kwa kipindi cha miezi minne iliyopita na kumfanya kuzima baadhi ya ndoto zake baada ya kufunga mabao 28 katika mechi 46.

Ibrahimovic atavaa jezi namba 10 ambayo iliachwa wazi na mshambuliaji Wayne Rooney ambaye kwa sasa amejiunga na Everton.


Comments