Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Manchester city Stevan Jovetic amesaini Monaco miaka 4.
Jovetic aliyehusishwa na usajili wa Newcastle amejiunga na timu hiyo ya league 1 kwa ada ya uhamisho wa pauni 10 milioni kutoka Inter Milan.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 amekabidhiwa jezi 10 ambayo imeachwa na Kylian Mbappe ambaye atajiunga na PSG.
Jovetic aliichezea Manchester city michezo ndani ya misimu miwili na kufunga mabao 8.
Pia fowadi aliwahi kuwa kipaumbele cha kocha wa sasa wa Newcastle Rafael Benitez (wakati huo akiwa kocha wa Liverpool) ambaye alitaka kumsajili mchezaji huyo alipokuwa na Fiorentina mwaka 2009.

Comments
Post a Comment