Liverpool imethibitisha kukamilika kwa usajili wa kiungo Naby Keita ambaye atajiunga na timu hiyo msimu ujao.
Kwa mujibu wa Sky sports Liverpool italipa kiasi cha £48 milioni ambayo haitakuwa ada rasmi moja kwa moja.
Kiungo huyo alifanyiwa vipimo siku ya jana na tayari alimalizana na Liverpool, atajiunga rasmi na timu hiyo Julai 1 hapo mwakani.
Keita mwenye miaka 22 atavunja rekodi ya usajili ambayo iliwekwa na Mohamed Salah aliyetua Liverpool kwa dau la £39.9 milioni akitokea AS Roma ya Italy.

Comments
Post a Comment