Usajili umezidi kushika kasi barani na tayari mchezaji wa PSG Blaise Matuid ametua Jijin Turin kufanya vipimo ili kukamilisha usajili.
Matuidi mwenye miaka 30 alijunga na PSG mwaka 2011 akitokea St Etienne, mchezaji huyo alicheza mechi 34 msimu uliopita na kufunga mabao 4.
Tayari usajili wa Neymar ambaye ametua kwa dau la £198 umefungua njia kwa mchezaji kujiunga na bibi kizee wa Turin na atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Juventus.
Usajili mwingine uliokamilika ni wa kiungo Gylf Sirgurdsson ambaye amejiunga na Everton akitokea Swansea kwa ada ya uhamisho wa £45 milioni.


Comments
Post a Comment