DR Kapinga abeba nafasi ya Mgosi Simba.


Aliyewahi kuwa Daktari wa zamani wa Klabu ya Simba Dk. Cosma Kapinga ametangazwa kuwa meneja mpya wa wekundu hao.

Kapinga ndiye mrithi wa Mussa Hassan Mgosi ambaye amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu hiyo.

Mgosi amepewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Vijana sambamba na mkongwe mwenzie Nico Nyagawa.

Kapinga ataanza rasmi majukumu yake muda mfupi baada ya kurejea nchini kwa kikosi cha timu hiyo ambacho kimepiga kambi Sauz.

Comments