Giroud, Ramsey wainyanyua Arsenal maji ya jioni.


Timu ya Arsenal imeupokea vizuri msimu mpya wa ligi ya England baada ya kuichapa Leicester city mabao 4-3.

Hadi kufikia dakika ya 80 Leicester ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-2 hata hivyo Ramsey na Giroud waliotokea benchi walikuja kubali hali mchezo.

Mchezaji Aaron Ramsey alisawazisha bao la tatu katika dakika ya 83 na Oliver Giroud alipeleka pointi 3 Emirates baada ya kutupia nyavuni bao la nne la ushindi katika dakika ya 85.

Pia mshambuliaji mpya aliyesajiliwa katika timu Alexandre Lacazzate alifungua ukarasa wa mabao ligi na katika timu ya baada ya kufunga bao la kwanza katika dakika ya 52.

Comments