Hakuna anayetaka Coutinho aondoke Liverpool.


Kiungo wa Liverpool Giorginio Wijnaldum amesema kuwa hakuna anayetaka Coutinho aondoke kwenye timu hiyo.
                     Giorgino Wijnaldum

Wijnaldum aliyasema hayo jana alipokuwa akihojiwa na Sky sports baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim.

"Kila mmoja anapenda Coutinho abaki, hakuna mtu wa kumpangia nini afanye.

"Kuondoka ni maamuzi ya mtu, anatakiwa kufanya maamuzi yeye binafsi." Alisema Wijnaldum

Coutinho alituma maombi akiitaka Liverpool imeuachie ajiunge na Barcelona hata hivyo Liverpool ilikataa kwa mara ya pili ya £90.4 milioni ambayo iliwekwa mezani na Barcelona.

Comments