Jesse ailaza vibaya Arsenal, Stoke ikishinda 1-0.


Mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal imelamba joto ya jiwe katika uwanja wa Brittani baada ya kufungwa bao 1-0 na Stoke city.

Bao pekee la Stoke city liliwekwa wavuni na Jesse Rodriquez ambaye aliunganisha pasi ya Saido Berahino katika dakika ya 71.

Arsenal ambayo ilipata wakati mgumu dhidi ya Leicester city katika mechi ya ufunguzi imeruhusu kipigo cha kwanza leo.

Timu hiyo inajiandaa kusafiri katika jiji la Liverpool wikiendi ijayo kwa ajili ya mchezo utakaofata kwenye ligi ya England.

Comments