Beki wa kimataifa wa Uganda Juuko Murshid amerejea Simba baada ya kuhusishwa na uhamisho katika timu ya Orlando Pirates ya Sauz Afrika.
Mwenyekiti wa kamati ya Simba pamoja na mdhamini wa timu Mohammed Dewji wakionekana na mchezaji huyo jana na kuwatoa hofu mashabiki wa Simba.
Kwa upande wa Hans Poppe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba alisema kuwa mshabiki waondoe wasiwasi kwani mchezaji huyo hatajiunga na Yanga kama ilivyodhaniwa.
"Nataka niwaotoe hofu mashabiki wa Simba kuwa Juuko amerejea Tanzania, na ataendelea kubaki Simba na wala hatajiunga na Yanga kama inavyodhaniwa."
Hans Pope aliongeza kuwa beki huyo walimpatia ruhusa maalum ya kwenda kwenda kufanya majaribio nchini Sauz.
Juuko ataungana na wachezaji wa kikosi cha Simba ambao wameweka kambi maalum visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya wapinzani wao Yanga.

Comments
Post a Comment