Kocha wa Azam FC Aristica Cioaba amesema kuwa kambi ya siku kumi waliyoweka nchini Uganda imempa kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo.
Azam FC iliweka kambi jijini Kampala nchini Uganda na kucheza mechi tano za kujipima nguvu dhidi ya KCCA ambao ndiyo mabingwa, Vipers, Onduparaka, URA na The Cranes kikosi cha ndani.
Timu hiyo haijapoteza mtoto wote ilipokuwa nchini baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na KCCA, ushindi wa bao 2-0 dhidi ya URA, ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Onduparaka, na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya The Cranes wachezaji wa Ndani.
Aristica alisema kuwa mechi hizo zimeleta morali kikosi na kuwajenga wachezaji uwezo wa kujiamini wakiwa uwanjani.
"Mechi hizi ni muhimu, tumejenga wachezaji morali yao na kuingiza mbinu za kiufundi ambazo wachezaji wamezingatia, hatujapoteza mchezo wowote." Alisema Kocha huyo.

Comments
Post a Comment