Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amependekeza kuwa bado Liverpool inahitaji kusajili baada ya kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Klopp ana imani kuwa hatua waliyofikia Liverpool kwa sasa kuna kila dalili ya kujenga ushawishi kwa wachezaji ili kujiunga na wababe hao Anfield ambao kwa upande wao imekuwa nadra sana kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa miaka ya hivi karibuni.
Liverpool wameionda Hoffenheim kwa ushindi wa mabao 6-3 kwa mechi za nyumbani na ugenini, katika mchezo wa kwanza Liverpool ilipata ushindi wa mabao 2-1 nchini Ujermani na jana ilipata ushindi wa mabao 4-2 katika uwanja wa Anfield.
Mohamed Salah, Dominic Solanke na Andy Robertson ndiyo wachezaji pekee ambao Liverpool imesajili mpaka sasa katika dirisha hili la usajili.
"Hii ni ligi ya mabingwa Ulaya, tumefuzu, tumekuwa kivutio kikubwa katika soko la usajili." Anasema Klopp
"nilisema si vizuri kuongelea wachezaji kabla ya mchezo ndiyo njia pekee ya kupata wachezaji walio bora kuliko tulionao. lakini jambo kubwa linalonipa furaha ni kufuzu katika hatua ya makundi." aliongeza Meneja huyo.

Comments
Post a Comment