Kocha wa Yanga atimka nyumbani kwao.


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga George Lwandamina ameondoka nchini kuelekea kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia.

Kwa mujibu wa blog ya Salehjembe kocha huyo ameondoka kwao kutokana na kufiwa na baba yake mzazi.

Yanga imethibitisha kuondoka kwa kocha huyo kutokana na matatizo ambapo kikosi cha timu hiyo kitakuwa chini ya Shadrack Nsajigwa ambaye ni kocha msaidizi.

Comments