Usajili live barani Ulaya leo.


Leo Agosti 30 ndiyo mwisho wa kusajiliwa kwa wachezaji kwenye ligi mbali mbali barani Ulaya, ambapo kufikia  majira saa 23.59 utakuwa muda wa mwisho kusajiliwa kwa wachezaji.

Eskaone blog inakueletea dondoo mbali mbali za usajili, na kukuhabarisha kwa kila kitachojiliwa kuanzia sasa mpaka dirisha litapofungwa

Story zilizotrend mpaka sasa

Chelsea imepekela ofa ya £25 milioni kwa Everton kumsajili kiungo Rose Barkley ambaye yupo kwenye majeraha kwa sasa.

Kwa mara nyingine ofa ya £50 milioni ambayo ilitolewa na Manchester city kwa ajili ya usajili wa Sanchez imecholewa na Arsenal.

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsajili mshambuliji wa Liverpool Divock Origi ili kuziba pengo la Dwight Gayle.

Las Palmas inataka kumsajili Diego Costa kwa mkopo mpaka mwezi January hapo mwakani atakaporejea Atletico de Madrid.

Spurs inajiandaa kumpatia Visa beki wa PSG Sergi Aurier ili kukamilisha usajili wake kwa ada ya uhamisho wa £23 milioni.

Everton huenda wakakamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji Stefano Okaka kutoka Watford.

Chelsea wapo mbioni kumsajili mshambiaji wa zamani wa meneja Antonio Conte Fernando Lloriente ambaye aliwahi kunolewa na Meneja alipokuwa Juventus.

Comments