Liverpool inavyotamba mbele ya Arsenal kwa rekodi hii.


Mambo yanazidi kunoga katika ligi ya England, wikiendi hii kutakuwa na mchezo mkali kati ya Liverpool na Arsenal katika uwanja wa Anfield.

Habari njema kwa mshabiki wa Arsenal ni kurejea tena uwanjani kwa mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye kwa mujibu wa meneja Arsene Wenger atakipiga katika uwanja wa Anfield.

Arsenal wanayo furaha kurejea kwa Sanchez lakini Liverpool watakuwa kiburi kutokana na rekodi yao waliyotamba nayo msimu uliopita dhidi ya timu 6 za juu.

Liverpool ilikuwa pekee ambayo haikupoteza mechi ya yoyote dhidi ya Chelsea, Manchester city, Manchester United, Arsenal na Tottenham.

Liverpool kwa kiburi chao ndiyo walioshikiria rekodi kushindi mechi 5 wakapata sare 5 bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya matembo wa England.

                        Rekodi ya Klopp

Liverpool ilikusanya jumla ya pointi zikiwemo pointi 6 za Arsenal ambayo ilikubali kipigo nje na ndani ambapo mechi ya kwanza walipoteza Emirates baada ya kufungwa bao 4-3, na katika mechi ya Anfield Liverpool ilishinda bao 3-1.

Ingawa mpira ni matokeo ya dakika 90 lakini wachambuzi wengi wametoa asilimia kubwa kwa Liverpool huenda wakaondoka na pointi dhidi ya Arsenal kutokana na rekodi yao.

Bado wachambuzi wanasema kuwa huenda Arsenal ikapata matokeo pia kutokana na mfumo wa sasa wa 3-4-3 ambayo unaonekana kupewa kipao mbele na meneja Wenger alipowadhibiti Manchester United.

Mfumo huo unaonekana una nguvu kwa upande wa Arsenal ambayo pia ilipata ushindi katika finali ya FA dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley.

Swali linabaki kuwa mfumo 3-4-3 utainyanyua Arsenal mbele ya Liverpool ambayo ina mawinga wenye kasi kama Sadio Mane na Mohamed Salah? Kwa mujibu wa Jamie alipichambua Chelsea dhidi ya Spurs msimu uliopita, Carragher anasema kuwa njia pekee ya kuifunga Chelsea ni kutumia eneo la wazi.

Ni lipi eneo eneo la wazi kwa Arsenal, nadhani eneo linatowaliwa na back-wings lakini ni eneo ambalo Sadio Mane na Mohamed Salah wanatokea bila shaka Wenger anatakiwa kujipanga vizuri.

Comments