Timu ya Liverpool imeanza na safari ya matumaini kuelekea kwenye makundi ya UCL baada ya kuichapa Hoffenheim bao 2-1.
Liverpool imepata ushindi huo ugenini bado itakuwa na kibarua cha kupata ushindi katika uwanja wa Anfield ili kujihakikishia nafasi ya kuingia kwenye makundi.
Kinda anayechipukia Liverpool Alexander Anold ndiye aliyeanza kuiweka mbele timu hiyo baada ya kufunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 35 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Liverpool ilifanikiwa kupata bao la pili kutokana na shambulizi la James Milner na kumfanya beki Hoffenheim kujifunga bao la pili katika dakika ya 75.
Hata hivyo Hoffenheim walipata bao la kufutia machozi baada ya mshambuliaji aliyetokea benchi Mark Uth kuifunguia bao timu yake katika dakika ya 87.
Pamoja na Hoffenheim kutawala muda mwingi kwenye mchezo lakini walishindwa kuzuia kipigo katika uwanja wa nyumbani.

Comments
Post a Comment