Mambo yamezidi kuwa magumu kwa kocha Arsene Wenger baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool.
Liverpool ilitawala soka kwa vipindi vyote viwili na kuipoteza Arsenal katika eneo la katikati ambalo lilionekana kutawaliwa ipasavyo na Emre Can, Jordan Henderson na Giorginio Wijnuldum.
Mabao ya Liverpool yalizamishwa nyavuni na Roberto Firmino katika dakika ya 17, Sadio Mane dakika ya 40, Mohamed Salah dakika ya 57 na Daniel Sturridge dakika ya 77.

Comments
Post a Comment