Lwandamina alamba mkataba mpya Yanga SC.


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC hawana mpango wa kuachana na kocha wao George Lwandamina baada ya kumuongeza mkataba mpya.

Lwandamina mwenye asili ya Zambia atasaini mkataba huo baada ya kumalizika kwa ule mkataba wa awali.

Yanga kupitia katibu wake Bonifas Mkwasa imesema kuwa wameridhishwa na uwezo uliooneshwa na mzambia huyo na hivyo hawana budi kumpa mkataba mpya.

"Tumejitahidi kuboresha maslahi kwenye mkataba huo ili kumpa motisha kocha wetu na timu iendelee kufanya vizuri zaidi." Alisema Mkwasa.

Ndani ya mwaka mmoja kocha huyo aliweza kuipatia Yanga taji la ligi kuu ya Vodacom pamoja na kuiongoza timu hiyo kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la FA.

Comments