MAJANGA: Suarez ataikosa Barcelona Mwezi mzima.


Barcelona huenda ikapitia wakati mgumu itakapoanza ligi wikiendi bila Luis Suarez ambaye atakaa nje uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.

Suarez aliumia goti katika mchezo wa jana dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Barcelona imethibitisha kuwa mchezaji huyo atakuwa nje ya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kupokea ripoti ya daktari.

Suarez mwenye miaka 30 ataungana na beki Gerard Pique ambaye na yeye aliumia hapo jana, huenda akamaliza mwezi mzima nje ya uwanja.

Comments