Mambo si Mambo kwa Singano Messi.


Winga wa Tanzania Ramadhan Singano 'Messi' ambaye alijiunga Difaa Al Jadida yupo njiani kurejea nchini.

Zipo taarifa kuwa Benchi la ufundi la Al Jadida hawajaridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo imeripoti blog ya Saleh Jembe.



Benchi la klabu hiyo linamuona Singano ni mchezaji ambaye kiwango chake  hakitofautini na baadhi ya wachezaji waliopo Al Jadida.

Kwa mujibu wa tovuti ya Shaffih Dauda imeelezwa kuwa wakala wa Singano ndiye aliyechangia hali hiyo kutokana na kujawa tamaa.

Taarifa za karibu zimeeleza kuwa wakala huyo ameonyesha tamaa ya kuongeza fedha ambayo haikuwepo kwenye makubaliano kama ilivyopangwa hapo awali.

Messi anawahi nchini kusaka klabu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na huenda akarejea Al Jadida endapo wataonesha nia ya kumuhitaji.

Comments