Kampuni ya G Trucks $ Equipment LTD imeotoa kiasi cha shilingi milioni 148 kuidhamini Mbao FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa Kulwa Bundala ambaye ni meneja masoko wa kampuni hiyo amesema kuwa udhamini unataambatana na udhani wa basi la timu hiyo lenye thamani ya shilingi milioni 70.
Bundala alisema kuwa wamemua kuitangaza kampuni yao kupitia Mbao kwa kuwa ni moja ya timu ambayo ilifanya vizuri kwenye ligi kuu Vodacom msimu uliopita.
"Jumla ya udhamini ni shilingi milioni 140 ikiwemo milioni 70 walizonunulia basi hilo na kiasi cha fedha kinachobaki ni kwa ajili ya matumizi mengine." Alisema Bundala.
Kwa upande wa Mbao kupitia mwenyekiti wao Solly Nyashi wameishukuru kampuni hiyo kutokana na udhamini mkubwa walioufanya.

Comments
Post a Comment