Messi atupia 2, Barca ikibeba pointi 3 mbele ya Alaves.


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameonesha bado yuko moto baada ya kufunga mabao 2, katika ushindi wa bao 2-0 waliopata dhidi ya Alaves hapo jana.

Messi alizamisha wavuni bao la kwanza katika dakika ya 55 na bao lingine alifunga katika dakika ya 66.

Ushindi wa Barcelona umeanza kutoa changamoto kwa mabingwa wa ligi kuu nchini humo Real Madrid ambao watapambana na Valencia katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Comments