Klabu ya Yanga imedai kuwa bado wapo kwenye wakati mgumu kuishawishi Azam kumuachia beki wake wa kushoto Gadiel Michael.
Katibu mkuu wa Yanga Bonifas Mkwasa amethibitisha kuwa tayari Michael alishasaini Yanga lakini Azam imegoma kumuachia wakidai bado wana mkatana na beki huyo.
Mkwasa aliongeza kuwa taarifa walizopokea awali zilionesha mchezaji alimaliza mkataba na Azam lakini beki huyo mkataba wake unamalizika mwezi Desemba mwaka huu.
Akizungumzia malipo ya ada ya uhamisho wa mchezaji huyo Mkwasa alieleza kuwa wamepokea barua kutoka Azam na hivyo wameshindwa kufikia kiasi cha malipo ambacho ramba ramba wamehitaji Yanga iwalipe na kuongeza kuwa watasubiri hadi muda wake utakapomalizika.
Pia katika huyo alidai kuwa Yanga imekuwa ikiwafanyia figisu kila wanapohitaji mchezaji kutoka Azam hali ambayo imekuwa kwa wapinzani wao Simba ambao wanadaiwa kuchukua wachezaji kiulaini kutoka Azam FC.

Comments
Post a Comment