Mwamuzi ajitangaza kuwa shoga England


Mwamuzi wa chama cha soka England Ryan Atkin ameamua kutangaza wazi msimamo wa maisha maisha yake kuwa yeye ni shoga.



Atkin mwenye miaka 32 amesema kuwa kuwashirikisha watu hadithi yake ni hali inayoleta matumaini hasa kwa kipindi hiki ambacho chama cha soka England (FA)  kimeweka msimamo wake kuwasapoti wapenzi wa jinsi moja.



Vyama vinavyosimamia mshindano ya FA, Ligi kuu na EFL viliweka wazi msimamo wake wa kuwapigia debe kundi hilo na kuwatetea pale wanapopingwa kupitia kampeni ya Stonewall's Rainbow Laces.

Atkin ameiambia Sky sports "kuwa vile unavyotaka kuwa na kubali wengine jinsi walivyo" ikiwa ni sehemu ya msisitizo wa kukubaliana na jinsi alivyo.


England imekuwa moja ya nchi ambayo bado inawataka watu wa mtazamo huo kuweka wazi jinsi walivyo ili waweze kushiriki kwenye kazi zao soka bila kutengwa.

Comments