Timu ya Mtwara Ndanda FC imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Motisun Group kupitia bidhaa yao ya kiboko.
Kwa mujibu wa Motisun Group udhamini huo una thamani sawa na ule wa mdhamini wa ligi kuu Vodacom.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mshauri wa masoko na biashara wa Ndanda Peter Simon alisema kuwa anaishukuru Motisun kwa udhamini huo ambao utawawezesha kupambana na changamoto za ligi kuu.
Simon aliongeza kuwa udhamini huo utawawezesha kusafiri katika mechi za ugenini ambazo watacheza nje ya uwanja wa Nangwanda Sijaona.
"Niwaahid Motisun Group bidhaa yao ya kiboko tutaitangaza vema kupitia timu yetu inayoshiriki ligi kuu.
"Ndanda kupitia timu yetu tutaongeza wateja kwa kuitangaza vema bidhaa ya kiboko." Alisema Simon


This comment has been removed by the author.
ReplyDelete